Baada tu ya matokeo ya uchaguzi wetu kutangazwa, nchi ilikumbwa na ghasia, ambazo zilihathiri sehemu nyingi za Kenya, hasa katika maeneo ya wakaaji ni wa makabila tofauti.

jacquekine

Mthidi wa ubakaji unaohusiana na mzozo kutoka Kenya

Baada tu ya matokeo ya uchaguzi wetu kutangazwa, nchi ilikumbwa na ghasia, ambazo zilihathiri sehemu nyingi za Kenya, hasa katika maeneo ya wakaaji ni wa makabila tofauti.

Mahali nilipokuwa naishi, zilikuwa Nyumba tatu kwa ploti hiyo moja. Usiku mmoja, wakati ghaasia zilipokuwa zimeanza, rafiki wa jirani alikuja akigonga gate yetu,akiongea kwa hisia nyingi na uoga kwamba alikuwa akitoroshwa na polisi. Aliomba nimufungulie mlango, ndio asishikwe na polisi waliokuwa wanzuru maeneo wakishika doria, na kuniomba nimruhusu ndani, ajikinge kwa muda. Alitaka kusubiri hadi doria ipite kabla ya kuenda kwake.

Nilimruhusu ndani, lakini mara tu alipoingia, niligundua kua alikuwa na nia mbaya. Akaanza kunishika kwa lazima huku nikimusukuma. Tulikabiliana vikali na sikutaka kuamusha Watoto. Akanizidia nguvu na kuweza kunidhulumu kimapenzi, yaani kunibaka.  Hatimaye, mwezi mmoja baadaye, niligundua kuwa nilikuwa mjamzito—Nakukumbuka hii ilikuwa karibu tarehe 16 Januari. Tarehe 16 Februari nilidhibitisha kuwa nilikuwa mja mzito. Hiyo ilikuwa changamoto kubwa sana kwangu!

Nilimruhusu ndani, lakini mara tu alipoingia, niligundua kua alikuwa na nia mbaya. Akaanza kunishika kwa lazima huku nikimusukuma.

jacquekine

©2024 Jadwiga Brontē & Jacquekine Mutere

Let’s Talk About Rape® ni mradi wa ushirikiano na tiba unaowawezesha waathiriwa kudai upya simulizi zao. Kupitia upigaji wa picha za kujipiga kwa kutumia kebo ya kutolewa kwa kipiga picha, washiriki huweka ajenda zao wenyewe kama chombo cha uponyaji.

Jacqueline. Kisumu, Kenya, 2024

Nilijaribu kutoa hiyo mimba mara tatu, lakini kila jaribio lilishindwa. Hatimaye, nilijifungua. Mara tu baada ya kujifungua , nililazimika kurudi hospitalini kwa sababu nilipata sepsis kutokana na upasuaji was ceaserean niliopitia.  Kuanzia Novemba 2008 hadi Januari mwaka uliofuata (2009), nilikuwa hospitalini nikipona. Hizo miezi tatu, nilitumia hiyo muda hospitalini kutafakari juu ya Maisha yangu, na kupona. Nilifanyiwa upasuaji takriban mara tatu, kuondoa maambukizi kutoka kwenye sehemu yangu ya upasuaji.

Wakati wa upasuaji wa mwisho,nilihofiya Maisha yangu, pia ya watoto wangu. Baada ya kuingia ndani ya chumba cha upasuaji, nilifanya agano na Mungu, nikimuomba anihifadhi na watoto wangu, kwani nilikuwa na wengine watatu nyumbani. Sikuweza kuamini kwamba kitu chochote kikinifanyikia, Watoto wangu wadhulumiwe. Niliomba Mungu, na Niliapa kutumia sauti yangu itumike kuangaazi dhuluma hasa zaidi kwa wale wanaoogopa kuonekana kwa ajali ya kudhulumiwa.Niliomba Mungu haya ikiwa nitaweza kuishi.

©2024 Jadwiga Brontē & Jacquekine Mutere

Let’s Talk About Rape® ni mradi wa ushirikiano na tiba unaowawezesha waathiriwa kudai upya simulizi zao. Kupitia upigaji wa picha za kujipiga kwa kutumia kebo ya kutolewa kwa kipiga picha, washiriki huweka ajenda zao wenyewe kama chombo cha uponyaji.

Jacqueline. Kisumu, Kenya, 2024

Operesheni ilienda vizuri na nikaanza kupona

Baada ya kupona na kupata ushauri nasaha, nilikutana na waathiriwa wenzangu, wanawake na wasichana . Tulijiuliza ni nani anayezungumza kwa niaba yetu? Hii ni baada ya kufanya kazi na Tume ya Ukweli, Haki, na Maridhiano . Tulikutana na waathiriwa wengi ambao walidhulumiwa. Wengi walikuwa wametoka sehemu tofauti za Kenya na walikuwa wamehamishwa katika maeneo mbalimbali au kambi, ambapo ghasia za kijinsia zilikuwa nyingi.

Siku moja, sikuweza kuhudhuria mkutano niliokuwa nimealikwa. Nikaomba msichana muadhiriwa mwenza kuhudhurria kwa niaba yangu. Ingawa hatukuwa tumekutana ana kwa ana kabla, alikubali. Baada ya mkutano, hatimaye tulikutana, nikatembelea nyumbani kwake, na kuweza kuwa marafiki wakubwa. Niliona mtoto wake msichana mdogo  nikiwa na ufahamu kwamba wote wawili walikuwa waathiriwa. Mtoto alikuwa mnyonge, njaa, vipele vya ngozi na afya mbaya. Moyo wangu ulijaa huruma kwao kwa sababu msichana mdogo hakuwa na familia ya kumsaidia.

Jacqueline akichukua picha yake mwenyewe, Kisumu, Kenya ©2024 Jadwiga Brontē

Barabarani. Kenya ©2024 Jadwiga Brontē

Jacqueline akiwa nyuma ya pazia, Kisumu, Kenya ©2024 Jadwiga Brontē

Kidogo kidogo, nilianza kukusanya akina mama na watoto wao nyumbani kwangu kwa majadiliano kuhusu kile tunaweza kufanya pamoja. Tulitaka kuomba serikali usaidizi, kwani tuliweza kuona kwamba watu waliohamishwa kwa ndani walikuwa wakipata msaada wakati sisi, waathiriwa wa dhuluma za kijinsia, tuliwachwa inje. Tulianza tukiwa wanne, kila mmoja akiwa na mtoto aliye zaliwa kutokana na dhuluma. Hata hivyo, niliweza kushuhudia Watoto wakiwa wanacheza kando yetu hapo, wakitukanana na kuitana majina mbaya na chafu. .Nilielewa kwamba kusaidia watoto bila kushughulikia matatizo ya akina mama zao hakutaleta mabadiliko ya kudumu.

Hapa ndipo nilipoamua kuzingatia wanawake na akina mama badala yake. Tulianza kuunda chama chetu Grace Agenda likiwa shirika la waathiriwa kuweza kutetea waathiriwa kwa ujumla. Mara nyingi tulialikwa kwenye mikutano, tuliondoka  bila chochote cha maana kusaidia wenyewe. Tuligundua kwamba tulihitaji kutetea mahitaji yetu na kutafuta suluhu. Katika miaka iliyopita, tumekua; sasa tuna ofisi na tumepiga hatua kupitia mafunzo na Kituo cha Kimataifa cha Haki za Mpito.

Leo, tunawakilisha takriban waathirika 298 nchini waliojiandikisha na Grace Agenda. Kwa bahati mbaya na hali ya maisha, wengine wamefariki, ikiwa ni pamoja na mwanamke mmoja ambaye hakuwahi kuona manufaa ya kuwa sehemu ya Grace Agenda, lakini natumai watoto wake watafaidika siku moja kutoka kwa mapambano yetu ya haki.

Baada ya upasuaji, niliposikia mtoto akilia, nilidhani nesi wanapaswa kumtunza huyo mtoto anayelia. Ni pale nilipogeuka kitandani, na kuona kifurushi kidogo cha kijani kilichokuwa kando yangu ndipo niligundua kilio cha mtoto kilikuwaa cha mtoto aliyekuwa wangu.

jacquekine

Nahitaji pia kutaja mtoto wangu, Princess, ambaye awali sikuwa na hamu naye lakini sasa ni mrembo wa umri wa miaka 16. Nilimuita Princess kwa sababu yan jia ya kifalme aliweza kuepuka kifo na kutoka msichana mrembo, zaidi ya mipango yango kumuondoa duniani. Baada ya upasuaji, niliposikia mtoto akilia, nilidhani nesi wanapaswa kumtunza huyo mtoto anayelia. Ni pale nilipogeuka kitandani, na kuona kifurushi kidogo cha kijani kilichokuwa kando yangu ndipo niligundua kilio cha mtoto kilikuwaa cha mtoto aliyekuwa wangu. Papao hapo, baada ya kufungua hicho kifurushi, moyo wangu ulibadilika, na niliamua kumwita Princess, na pia kwa heshima ya mama yangu, Bernadette. Mara nyingi tunamwita Jasmine B, lakini kwa kawaida, tunamwita Princess au Becky.

Tunazidi mbele na kufwatilia na kutarajia Haki siku za usoni.

Hii ndiyo hadithi ya Grace Agenda.